The House of Favourite Newspapers

DC Gairo Atembelea Kijiji cha Kisitwi

 

 


Na Dustan Shekidele, Global Publishers |Morogoro

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shahidi Mchembi  akiwa viongozi wengine wilayani humo wametembelea Kijiji cha  Kisitwi kwa ajili ya kuhimiza maendeleo. 

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Shahidi Mchembi akiwa ofisini kwake.

Tukio hilo limetokea wiki iliyopita wilayani humo ambapo mkuu huyo wa wilaya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Clement Mjulwa, Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya, Abdi Ndilla na Katibu Tawara wa Wilaya, Adam Bibangaba walifika kijijini hapo na kufanikiwa kuzungumza na wananchi wakihimiza maendeleo, uchapa kazi.

DC Mchembi akipanda kwenye gari lake.

Aidha DC Mchembi alifika katika Shule ya Msingi Kiswiti liliyopo kijijini hapo Kata ya Lubeho umbali wa takribani kilomita 20 kutoka Gairo Mjini na kukabidhi madawati 50 ya msaada yaliyotolewa na Bank ya Exim.

Kabla ya kufika shuleni hapo, msafara huo ulikwama  katikati ya msitu kufuatia barabara kukatika na magari kushindwa kupita,  hivyo DC Mchembi na msafara wake waliamua kushuka kwenye magari yao na kutembea kwa miguu umbali wa takribani mita 200 ili kuvuka upande wa pili na kuendelea na safari yao.

Miundombinu ya barabara kuelekea Kijiji cha Kiswiti

DC Mchembi akipokelewa shuleni hapo.

Comments are closed.