The House of Favourite Newspapers

JINI MTU-08

 Nilikuwa mbele ya hospitali ya maweni, yapata saa tatu za usiku, nilikuwa nimefura kwa hasira na chuki kubwa dhidi ya binadamu mwenye kuitwa Hashimu Azizi.

Bindamu asiye pata kujulikana kwa urahisi kutokana na jina hilo la uficho alilokuwa akilitumia,.kila mara akili yangu ilikuwa ikirejea siku binadamu huyo alipokuja katika himaya yangu na kuhitaji msaada wangu ilihali  ni yeye huyo huyo mwenye kunipa tabu na mateso katika upande wa dunia,.

Niliumia mno.

Niliapa pale nitakapo mwingiza katika mikono yangu atajuta kunifanyia ubaradhuli katika dunia.

Nilizipiga hatua nikipita katika mageti yaliyo kaliwa na walinzi, hakuna mlinzi aliye nizua wala kuniuliza kitu gani nataka maeneo yale ya hospitali ilihali haukuwa muda wa kuona wagonjwa.

Wale walinzi wa hospitali ya maweni, Siyo walio onekana wenye kuona kitu ama mtu yeyote mwenye kupita katika mageti yale ya kuingia na kutoka katika hospitali ile ya maweni.

Nilizipiga hatua moyoni nikiwa na ari kubwa ya kumpata yule ninae msaka.

Niliingia ndani kabisa ya wigo wa hospitali ya maweni nikanyooka na kinjia kidogo kilicho sakafiwa vizuri kwa sakafu nzuri.

Nilinyooka na kile kinjia hadi kilipo kuwa kimeishia kwa kugawanyika pande mbili, njia moja ilielekea upande wa kulia ambapo kulikuwa ni wodi ya wagonjwa mahututi, huku kile kinjia kilicho elekea upande wa kushoto ilikuwa ni wodi ya wanawake, mbele kulikuwa na msingi uliotengeneza mtalo wa maji.

Niliuvuka ule mtalo wa maji kwa kuruka na kuelekea katika jengo liliokuwa mbele yangu ambapo kulikuwa na kibao kilicho kuwa juu ya mlango wa jengo hilo uliosomeka.

WODI YA MAITI.

Ukingoni mwa mlango wa kuingia ndani ya jengo hilo la kuhifadhia maiti kulikuwa na kibanda cha mlinzi ambaye alikuwa ndani ya banda hilo.

Nilisogea karibu kabisa na mlango wa lile jengo lenye kufahamika kwa jina la mochwari, palikuwa na kufuli kubwa.

Nilimtizama yule mlinzi ambaye alikuwa akinitizama upande ambao nimesimama lakini hakuonekana kuona mtu wa aina yoyote, niseme kuwa hapakuwa na binadamu ambaye angeweza kuniona kwa macho yake ya kibanadamu pasina kuwa na uwezo binafsi wa nguvu nyingine mbadala.

Nililitizama lile kufuli kisha nikazungumza maneno ambayo siwezi kuyataja, ni katika lugha ambayo HAIPO katika hii dunia, mara lile kufuli likachia ‘kwachaa’ likafunguka, nikasukuma mlango na kuingia ndani.

Kulikuwa na majokofu makubwa yaliyo tengenezwa kama droo za kabati katika ukuta,pia palikuwa na mwanga hafifu wa taa ya rangi iliyokuwa inawaka masaa ishirini na nne.

Nilijisogeza hadi katika droo iliyokuwa mwishoni kabisa ya chumba kile kikubwa, kisha nikavuta ile droo, macho yangu yakakutana na mwili uliokuwa umelala ukiwa umefumba kope ndefu kama za mdoli, midomo yake mizuri iliyo kuwa na lips zenye kukufanya utamani kuiona muda wote, midomo ilikuwa imepasuka kidogo kutokana na baridi lililokuwa katika lile jokofu, mashavu makubwa kiasi malaini yenye kupendezeshwa na ngozi ya rangi ya papai lililo iva ilimfanya kiasi uone mwanamke wa urembo kama ni aliye lala tu na siyo mfu {MAITI}.

Nilivuta hadi mwisho kabisa ile droo kisha nikamtoa Nasra wangu akiwa maiti yenye matundu mengi ya risasi.

Hasira zangu zilizidi kuwa kubwa mno, donge kubwa lilinikaba kooni, dhidi ya mshenzi Hashimu Azizi,.

“Hii vita ilikuwa ni kati yangu mimi na yeye sasa hawa viumbe wanahusika nini na haya?.”

Hasira zilikuwa zimenipanda katika kiwango cha mwisho kabisa.

Nilimnyanyua na kumweka katika mikono yangu kisha nikatoka nae nje, niliangaza huku na kule kuangalia namna ya kufika eneo nililo hitaji kueleka.

Nilipita katika njia ile ile niliyo ingilia nikipishana na watu wengi tu mule hospitali ya maweni pasina kuonekana kwa macho ya kawaida.

Upande wa mwanzo wa mageti ya kutokea nje kabisa ya wigo wa hospitali kulikuwa na maegesho ya magari ambayo karibu yote wamiliki wake walikuwa hawapo.

Hayakuwa na faida kwangu nikatoka nje kabisa ya hospitali ya maweni nikiwa nimembeba Nasra mikononi mwangu.

Nilivuka barabara na kwenda katika tax nyingi zilizo kuwa zimepaki mbele kidogo ya grosary nyingi ambapo palikuwa na watu wengi wakibwia pombe majira hayo.

Nilichagua tax moja na kufungua mlango kisha nikamwingiza Nasra na kumlaza vizuri siti ya nyuma, dereva tax alikuwa amekaa mbele ya boneti ya gari akifanya mawindo ya abiria.

Nilito kifaa kidogo katika mfuko wangu wa shati kilicho fanana na kishkizo cha chati,nikazungumza maneno ya kichawi katika kile kifaa kidogo na hapo simu ya yule dereva aliyekuwa nje ya gari ikaanza kuita.

“Yes hallow” alipokea kwa mbwembwe.

“Mambo Suka”, niliongea kupitia katika kile kifaa,huku kule kwa yule dereva ni sauti nzuri ya kike ndiyo iliyosikika katika simu yake. “poa bibie nani mwenzangu”

“Jamani kumbe namba yangu uliifuta”

Aagh..no siwezi kufuta namba ya mwanmke mwenye sauti nzuri kama wewe inawezekana nime save’ mara mbili thus way imekuja namba badala ya jina”

“Any way mimi Rukia nilitumia tax yako siku kadhaa nyuma nikachukua namba ili kama Napata tatizo la usafiri nakutafuta wewe..”

“Ok ok ok nambie mtoto mzuri” alidakia kwa kiherehere.. nikashangilia ushindi kwani tayari alishaingia katika kumi na nane. “now nipo bulega beach, njoo unichukue please”

“Ooh haina neno mrembo niaandalie elfu kumi na tano fasta naibuka hapo”

“Ntakupa ishirini wahi upesi jamani”

Nilimwona yule dereva alivyo furahia kuzipata elfu shirini usiku ule, aliingia katika gari na kuliwasha huku akifungulia muziki mkubwa wa bongo fleva.

Aliliondoa gari huku akitikisa kichwa kwa kuucheza muziki ule wa bongo fleva wenye mdundo mkubwa akiwa na furaha kwa kupata bingo la elfu ishirini, dakika ishirini na tano zilitosha kabisa kutufikisha mbele ya ufukwe za bulega, palikuwa kuna watu wachache mno usiku huo.

Yule dereva alisimamisha gari na kuchukua simu yake na kupiga katika ile namba ya mteja wake, sekunde saba badae akapata jibu lililo mchnganya kabisa yule mtu.

   “Namba unayo piga haipo tafadhali ichunguze namba hiyo kabla ya kupiga tena.

Aliichunguza tena vizuri ile namba katika simu yake kisha akipiga tena, lakini jibu likabaki kuwa lile lile, yule dereva alipiga ngumi uskani wa gari huku akitoa tusi kali languoni kutukana ile sauti iliyo mweleza anakosea namba.

Niliteremsha maiti ya Nasra kutoka katika ile tax ya yule dereva aliye patwa hasira za nyati aliye jeruhiwa kwa kuzikosa elfu ishirini huku akiwa amechoma mafuta yake bure bure.

Baada ya kuhangaika tena na tena kuipiga ile namba mwisho alichoka aliamua kuondoka.

Nilikaa chini pembeni mwa maiti ya Nasra, macho yangu yakiwa yanatizama kule ziwani kulikokuwa na giza zito na upepo wenye kusukuma mawimbi yaliyo jisukuma kwa kasi ukingoni na kutengeneza ukulele wa kufoka kwa maji, kwa mbali kukiwa na karabai nyingi za wavuvi zilizo onekana kama nyota ndogo mno katika anga.

Nilifumba macho yangu huku nikinuwia vitu fulani ilihali viganja vya mikono yangu vikiwa nimevikusanya pamoja, mbele yangu mita kama mia moja katika ziwa kuliibuka viumbe wanawake wenye kichwa cha mtu kiwiliwili cha samaki{nguva},walikuwa wanang’aa na kufanya eneo lote walipo ibukia kutengeneza mwanga mkali mno kama ule wa taa za malumu za kamera, mwanga ulioangaza hadi mahala nilipokuwa nimeketi mimi na maiti ya Nasra.

Wale viumbe waliogelea katika maji kusogea  eneo nilipokuwa nimekaa.

Walikuwa ni wanawake wenye sura nzuri mno, eneo lote lilipata mwanga wa ajabu mno, wale viumbe walitoa heshima kubwa mbele yangu kisha wakawa kimya kusikiliza maagizo.

Niliwatizama wale viumbe kwa makini, macho yao yalikuwa yakinitizama kwa hofu kubwa huku machozi yaliyo kuwa yakiwalenga lenga yalifanya moyo wangu upate kusita kidogo kwa kile nilicho kuwa nataka kukifanya dhidi yao.

Nilipeleka macho katika mwili wa mwanamke aliye kuwa amelala huku akiwa hana uhai nikapata msukumo kutenda lile nililo kuwa nimedhamilia,  nilitupa jicho kwa wale viumbe, sasa walikuwa wakitokwa na machozi kabisa hofu ikiwa kubwa mno moyoni mwao.

Sasa nikawa nashindana na nguvu mbili moyoni mwangu, nguvu ya kutwaa uhai wa wale viumbe, {samaki mtu} ili kugawa uhai wao kwa mwanamke wa kibinadamu ninae mpenda, wakati huo huo nikiwa na msukumo mwingine wa huruma dhidi ya wale viumbe niliotaka kuwateketeza ili mpenzi wangu apate maisha mengine katika ulimwengu.

Lazma hili lifanyike huyu mtu apate kuishi.. sitaki kuona hayo machozi mbele yangu,.haya futa upesi  niliwakoromea katika mawazoni kwa hasira wale samaki watu, na hapo nikaona wakitii kwa haraka wakaacha kulia na machozi yao  yaliyo kuwa yakitiririka katika mashavu yao yakayeyuka na kufutika kabisa.

Nilizungumza maneno fulani ya kichawi samaki mtu mmoja katika wale wanne, akaanza kugaa gaa chini huku akitoa yowe la maumivu makali mwilini mwake, na hata alivyo kuwa akipiga makelele yake, sauti yake ilisikika katika hali ileile ya mawazoni tu.

Badae kidogo alitulia, tayari alikuwa MAITI. Uuuuuuwiiiii” wale viumbe walipiga mayowe ya nguvu yaliyo kuwa katika hali ya hofu kuu.

  Kimyaaaaa nilifoka kwa ukali huku nimetoa macho makali yaliyo waogopesha wale viumbe.

Kimyaa.

Walitulia huku wakinitizama kwa jicho la mashaka makubwa, waliniogopa vibaya mno, nilikuwa najisikia vibaya mno hali ile lakini nguvu ya mapenzi ilikuwa kubwa mno.

Nani anafuata kufa?. Hili lilifanya wale viumbe watetemeke mno waliogopa kufa.

Nilakusanya viganja vya mikono yangu,nikazungumza yale maneno ya kichawi, nikaona furaha ya wale viumbe machoni hawakuamini kabisa kama nimeweza kuwaruhusu waondoke.

Walirejea katika maji huku pale chini akibaki kiumbe ambaye tayari alikuwa maiti, kukawa na giza zito, nilimgeuza yule samaki mtu{nguva} na kumlaza chali huku nikitawanya mikono yake.

Nilianza kunuia tena maneno mengine ya kichawi  ambayo yalinichukua muda mrefu mno, mara vitu vyenye kung’aa vilivyo kuwa kama unyoya laini wa ndege,vikatokea katika mdomo, pua na masikioni mwa yule kiumbe.

Vitu vile vyenye kufanana na manyoya laini ya ndege vikawa vina elea katika anga taratibu vikisogea katika mwili wa Nasra, viliuzunguka mwili wa Nasra halafu vikaanza kuingia katika mwili wake kupitia katika masikio mdomoni na puani.

Viliingia vyote.

Zilipita dakika mbili mara nikamwona Nasra anahema, nilisogeza sikio langu karibu na kifua chake, naam  hata mapigo yake ya moyo yalikuwa yakipiga.

“Nasra” nilimwita taratibu.

Kimya.

“Nasra niliita tena” huku nikimtikisa.

Kimya kingine.

“Nasraaaa” niliita kwa nguvu nikimtikisa kwa kasi Zaidi, macho yake yalifumbuka taratibu ikiwa ni kama kwamba ametoka katika usingizi  mzito.

“Abeee” alitika kwa sauti yake laini iliyo onyesha kabisa ametoka katika usingizi mzito.

Nilitabasamu moyo wangu ukipata furaha mno,nilimkamata mabega yake nikamkumbatia kwa mapenzi makubwa.

“Ni…ko wapi hu..ku”

“Tulia Nasra tulia mpenzi wangu uko na mimi,vegasi”

“Tuko huku toka saa ngapi? halafu mbona…!aagh na huyo aliye lala hapo ni nani?af..nini hii..mwanangu yuko wapi?,na huku ni wapi tena.?”

Aliuliza maswali mfululizo huku akili yake ikiwa na mawenge lukuki.

Nilihisi nitapata tabu sana kumwelewesha Nasra kwa muda ule mengi yaliyo tokea,  Zaidi kuhusu mtoto wake ambaye bahati mbaya  alikuwa tayari amekwisha zikwa.

Nilimtizama kwa jicho kali huku mionzi fulani kama shoti ya umeme ikitoka katika macho yangu na kuingia ndani ya kichwa chake, kisha nikachukua wajihi wa yule kiumbe {nguva} nikaipachika mbele ya uso wa Nasra.

Alipiga ukulele wa mstuko huku akirudi nyuma na kunitizama kwa mashaka makubwa, lakini ndani ya sekunde hiyo hiyo akili yake ikamruka na kuwa mwehu mwenye wajihi wa samaki mtu {nguva}.

Hii maana yake akae siku sita bila kuingiliwa kimwili, asile samaki wala nyama ama kitu chochote chenye asili ya damu damu,vinginevyo namkosa Nasra wangu,kwani amepungukiwa dutu{element} sita za uhai wa kiumbe mwenye kufufuliwa na miungu ya bahali.

Niliyafikilia mazingatio hayo huku nikimwona Nasra akifanya vitendo vya kiwenda wazimu kabisa.  sasa vipi nita mlinda na masihibu haya ilihali niko nae mbali kimwili.

Niliugeukia ule mwili wa nguva,nikanyoosha kidole cha shahada katika mwili ya yule kiumbe, hapo akaanza kuyeyuka katika maji mithili ya bonge la balafu liliwekwa katika jua, dakika moja  akapotea kabisa.

Nilipo geuza shingo yangu upande wa Nasra alikuwa akizidi kutokomea katika giza huku akiimba nyimbo za kiwehu wehu!.

Nikatuliza fikra zangu sekunde za kuhesabu kisha robo ya  fikra zangu zikawa kichwani mwa Nasra

 

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Jumatatu hapahapa.

Comments are closed.