The House of Favourite Newspapers

DC wa Ubungo Atoa Rai kwa NGO’s Kutoka Maofisini na Kwenda Kuwagusa Wananchi

0
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James

MKUU wa Wilaya ya Ubungo Kheri James leo Agosti 26, 2022 kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri amekutana na mashirika yasiyo ya kiserikali lengo likiwa ni kujadiliana kuwasilisha taarifa za mwaka ikiwemo miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa.

Akizungumza kwenye mkutano huo DC James amesema kuwa anatamani kuona mashirika hayo yasio ya kiserikali yanatoka maofisini na kuhakikisha kwenda kuwagusa wananchi moja kwa moja.

Kheri James amezitaka NGO’s kutoka Ofisini na kwenda kuwagusa wananchi moja kwa moja

Hadi kufikia Juni 2020 Manispaa ya Ubungo ilikuwa na mashirika 90 ambayo yamesajiliwa na kufanya kazi

 

Aidha Viongozi wa Mashirika hayo yasiyokuwa ya Kiserikali yameaswa kufanya kazi kwa kushirikiana na Maafisa Maendeleo wa Wilaya ya Ubungo ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Leave A Reply