The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Polisi wa Kitaifa Ajiuzulu Baada ya Kuuawa kwa Waziri Mkuu wa Japan

0
Mkuu wa Polisi wa Kitaifa wa Japan, Itaru Nakamura

MKUU wa Polisi wa kitaifa wa Japan, Itaru Nakamura amewasilisha ombi la kujiuzulu baada ya kukiri kushindwa kumlinda Waziri Mkuu wa zamani, Shinzo Abe ambaye aliuawa hivi karibuni wakati wa kampeni ya uchaguzi.

 

Nakamura ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa wameamua kupanga upya timu yao na kuanza misheni za usalama.

Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe

Shinzo Abe alifariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupigwa risasi Julai 8, 2022 wakati wa kampeni ya uchaguzi katika eneo la Nara lililopo Magharibi mwa Japani.

 

Mtu anayeshukiwa na mauaji hayo, Tetsuya Yamagami alikamatwa katika eneo la tukio na kwa sasa anafanyiwa uchunguzi wa kiakili hadi mwisho wa mwezi Novemba mwaka huu.

 

Yamagami aliwaambia polisi kwamba alifanya tukio hilo baada ya mama yake kuchangia pesa nyingi kwake na kumsababishia umasikini.

 

Siku moja baada ya kuuawa kwa Shinzo Abe, Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Nara, Tomoaki Onizuka alikiri kwamba kumekuwa na matatizo ya ulinzi na hatua za usalama za waziri mkuu huyo wa zamani.

Mshukiwa wa mauaji, Tetsuya Yamagami

Kutokana na tukio hilo Onizuka ameeleza kuwa jambo hilo lilitokea kwa ghafla na kutoa agizo kwamba uchunguzi zaidi ufanye ili kubaini kilichotokea.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply