The House of Favourite Newspapers

DCB Yatoa Gawio Kwa Wanahisa Wake Wakuu

0
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe; Selemani Jafo, akikabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya shilingi 138,603,889 ikiwa ni gawio la wanahisa kutoka Benki ya DCB kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godrin Gondwe (wapilikushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Zawadai Nanyaro, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe; Selemani Jafo (wa tatu kushoto), akikabidhi mfano wa hundi yenye dhamani ya shilingi 30,780,000 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga  ikiwa ni gawio la hisa za shirika hilo kutoka Benki ya DCB. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Zawadai Nanyaro, hafla hiyo imefanyika  jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa, akiwakaribisha Mkuu Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri,na Mkurugenzi wa Jiji Bi Sipora Jonathan  wakati wa hafla ya Benki ya DCB ilipokuwa ikitoa Gawio kwa wanahisa wake wakuu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati), akimsikiliza  Mkurugenzi Mtendaji  wa Mfuko wa Uwekezaji (UTT) Simon Migangala wakati wa hafla ya benki ya DCB ya kutoa gawio kwa wanahisa wake wakuu jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo Zawadai Nanyaro, 

 

Leave A Reply