The House of Favourite Newspapers

Denti Aliyetumbua ‘Boom’ Afungwa Jela Miaka Mitano

0

MWANAMKE mmoja wa Afrika Kusini, Sibongile Mani ambaye alifanya matumizi makubwa baada ya kupokea kimakosa fedha za ufadhili wa masomo takribani dola milioni 1 za Kimarekani (takribani shilingi bilioni 2.3) za Kitanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Mwanadada huyo alipokea Randi milioni 14 za Afrika Kusini badala ya Randi 1,400 alizostahili kupewa mwaka 2017 kwa ajili ya kulipia gharama za masomo kutoka kwenye Mfuko wa Mpango wa Kitaifa wa Msaada wa Kifedha kwa Wanafunzi (NSFAS).

Imeelezwa kwamba kupitia kampuni ya huduma za malipo ya Intellimali, Sibongile alipokea fedha hizo na hata alipogundua kwamba kulikuwa na makosa ya kuingiziwa kiwango kisicho sahihi, hakutoa taarifa kwenye mamlaka husika na badala yake alianza kuzitumbua kwa kufanya matanuzi.

 

Leave A Reply