The House of Favourite Newspapers

Diamond Aanika Album Yake Mpya ‘A Boy From Tandale’

MKALI wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameweka hadharani kuwa mnamo Machi 16 mwaka huu ataachia albamu yake mpya ya ‘A Boy From Tandale’ iliyobeba nyimbo 20 huku akifunguka kuwa wimbo namba 8 katika Albam hiyo inaeleza mambo mengi kuhusu maisha yake aliyopitia.

“Track namba nane #BAILA ni  miongoni mwa nyimbo zangu pendwa katika albamu ya Aboy From Tandale, nyimbo ambayo nimezungumzia mengi yenye uhalisia, yani inavyonifurukuta naona hiyo kama tareh 16 ni mbali…” ameandika Diamond kupitia Instagram.

Comments are closed.