The House of Favourite Newspapers

DIAMOND AMPELEKA HAWA KUTIBIWA INDIA

STAA wa Bongo Fleva, Daimond Platnumz, amesema anashughulikia taratibu za kumsafirisha msanii mwenzake, Hawa Said, ambaye aliwahi kumshirikisha kwenye wimbo wake wa ‘Nitarejea’ ili ampeleke nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

 

Kwa muda sasa, Hawa ameendelea kuishi kwa tabu na mateso makali baada ya kuambiwa na madaktari kuwa tatizo lipo kwenye ini,  hivyo linashindwa kupeleka na kusukuma maji mwilini, jambo ambalo limesababisha tumbo lake kujaa maji na kumfanya kwenda hospitali kila baada ya wiki mbili au tatu kwa ajili ya kunyonywa maji hayo wakati akisubiri matibabu zaidi.

Diamond ambaye ametoa kauli hiyo baada ya kuguswa na ugonjwa wa msanii huyo huku mashabiki wakimshutumu kwa kushindwa kumsaidia, hajaeleza ni lini safari ya kumpeleka Hawa nchini India itaanza na watakaa huko kwa muda gani.

Comments are closed.