Diamond Anunua Ndinga Mpya Cadillac Escalade Black -Video

Hii ni zaidi ya jeuri! Baada ya kuona maneno yamekuwa mengi, supastaa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz amemwaga ushahidi wa video wa juu ya kununua ndinga linguine jipya aina ya Cadillac Escalade Black Edition  jipya kutoka kwenye maganda yake.

 

Video mbalimbali zinaonesha gari hilo likifunguliwa kutoka kwenye kontena lililopelekwa hadi nyumbani kwake, Mbezi-Beach jijini Dar.

 

Hili linakuwa ni Cadillac Escalade ya pili kwa Diamond kununua ndani ya miezi miwili ukiachana na lile la kwanza lililosambaa mitandaoni wiki kadhaa zilizopita .

 

Cadillac ni gari ambazo wanamuziki wengi mabilionea wa nchini Marekani wanapenda kuyatumia. Pia linatumiwa na baadhi ya Marais wa nchi hiyo. Baadhi ya mastaa hao na Marais ni pamoja na Jay Z na Donald Trump.

Itoshe kusema kwamba ili uweze kuinunua gari hilo unahitajiku wa na mfuko uliotuna.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL


Toa comment