The House of Favourite Newspapers

DIAMOND APAGAWISHA MASHABIKI WIMBO WA ‘COLOURS’ WA KOMBE LA DUNIA 2018

MSANII wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku wa kuamkia leo amewapagawisha vilivyo mashabiki wake wakati akiimba wimbo maalum utakaosherehesha Kombe la Dunia 2018 wimbo uitwao Colours nyimbo aliyoshirikiana na Jason Derulo.

Hafla ya uzinduzi huo imefanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo ilikuwa ni uzinduzi wa Kampeni ya Mzuka Dimbani na Coka maalum kwa ajili ya Kombe la Dunia 2018.

 

Katika hafla hiyo Meneja wa Chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo, alisema kampuni ya Coca-Cola Tanzania ni moja ya mdhamini wa mashindano hayo makubwa ya soka duniani na inayofuraha kwa msanii kutoka Tanzania kushiriki kuimba wimbo maalum wa mashindano hayo na kwamba anaimani watanzania watapata mzuka wa soka dimbani na kujisikia sehemu ya mashindano.

 

Wimbo huo umetayarishwa na prodyuza Nahreel kwa kushirikiana na Ma prodyuza kutoka nchi nyingine.

Comments are closed.