The House of Favourite Newspapers

Diamond Ashindwa Kujizuia kwa Tiffah

0

DIAMOND Platnumz ameshindwa kabisa kujizuia na kukiri jinsi anavyompenda binti yake, Tiffah Dangote aliyemzaa na mwanamama Zari The Boss Lady.

 

Ukiwafuatilia kwa ukaribu utagundua kuwa Diamond na Tiffah wanapendana na kufuatiliana mambo yao kwa ukaribu licha ya kila mmoja kuishi katika nchi tofauti.

 

Wawili hawa hawaoneshi chochote kibaya zaidi ya upendo wakati wote licha ya Diamond kutengana na Zari. Ni wazi kuwa uhusiano wa Diamond na Zari hautarejea tena, lakini Tiffah yeye ana furaha na shauku ya kuwa karibu na baba yake.

 

Mara nyingi, Tiffah ameonekana akionesha baadhi ya sifa ambazo huchukuliwa kuwa maalum na urithi kutoka kwa baba yake huyo.

 

Kama tunavyojua, Diamond ni mwanamuziki mkubwa barani Afrika ambaye ushawishi wake umekuwa gumzo sehemu kubwa ya sayari hii ya Dunia.

 

Kwa kuangalia nyayo za Tiffah, unaweza kuona waziwazi ujasiri wake na huwenda akaja kuwa staa zaidi ya baba yake. Tukio bichi ni la wikiendi iliyopita ambapo Tiffah aliposti video ya baba yake huyo akifanya shoo huko Boston nchini Marekani.

 

Kwenye video hiyo, Tiffah alimpongeza baba yake kwa namna anavyopafomu kwenye tamasha. Hapo ndipo hatua ya Tiffah ikapata kibali machoni pa baba yake. Baada ya Diamond kuona ujumbe wa Tiffah alishindwa kujizuia na kumjibu akionesha jinsi anavyompenda. Diamond alimuandikia Tiffah: “Nakupenda sana Tee…”

Leave A Reply