The House of Favourite Newspapers

Ummy Ashusha Neema Gharama za Maegesho – Video

0

Serikali imepunguza faini ya kupitiliza muda wa malipo ya maegesho kutoka Sh30,000 hadi Sh10,000 huku muda wa malipo ukiongezwa kutoka Siku 7 hadi 14.

 

Mfumo wa malipo ya maegesho kielektroniki unatarajiwa kurejea tena Desemba mosi baada ya kusitishwa kwa muda kuanzia Oktoba 9.

 

Akitoa taarifa hiyo leo Ijumaa Novemba 5, 2021 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu ameagiza uhakiki wa madeni katika magari kabla ya mfumo huo kusitishwa. Amesema kuwa baada ya uhakiki wa madeni hayo mapendekezo yapelekwe Wizara ya Fedha.

 

“Madeni yanafikia Sh811 milioni, tunaangalia utaratibu wa kufuta madeni yaliyojitokeza kutokana na changamoto za mfumo huo, tunafanya uhakiki kisha yatafutwa kwa mujibu wa taratibu za Serikali” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

 

“Mfumo wa Kukusanaya ushuru wa maengesho (TeRMIS) umeshasimikwa na ulianza kufanya kazi katika Mikoa mitano ya Iringa, Singida, Mwanza, na ar es Salaam.

 

“Hata hivyo katika utekelezaji wa Mfumo wa TeRMIS tumepokea malalamiko ya uwepo wa kero kuhusu mfumo huo hususani kwa Mkoa wa Dar lakini tumeshayafanyia kazi.

 

“Kulikuwepo changamoto ya wateja kutopatiwa taarifa za kudaiwa ushuru wa maegesho kwa wakati, changamoto hii imetatuliwa na wateja watapatiwa ankara itakayoonesha muda, kiasi anachodaiwa, tarehe na eneo pindi watakapo tumia maegesho.

 

“Kero nyingine kubwa ilikuwa nikiwango kikubwa cha maegesho, kanuni za maegesho nimeziboresha, kwa Dar es Salaam mtumiaji wa maegesho atalipia Tsh 500 kwa saa na Tsh 2,500 kwa siku, tofauti na zamani ambapo mteja alipaswa kulipia Tsh 500 kwa saa na Ths 4,500 kwa siku.

 

“Hapo awali mtumiaji wa maegesho alitakiwa kulipa deni lake ndani ya siku saba tangu kutumia maegesho hayo kama hajalipa alitozwa faini mara mbili na akizidisha siku 14 hajalipa alitakiwa kulipa faini ya kile anachodaiwa pamoja na faini ya Tsh 30.

 

“Kuanzia sasa mtumiaji wa maegesho atalipa deni lake ndani ya siku 14, na atapewa taarifa, sidhani kama kutakuwa na kisingizio tena. Akishindwa kulipa ndani ya siku 14 hatatozwa faini ya Tsh 30,000 badala yake atatozwa faini ya Tsh 10,000. Adhabu ya Tsh 30,000 nimeifuta na ile ya kuongezeka mara mbili nimeifuta.

 

“Changamoto nyingine ilikuwa baadhi ya wateja kushindwa kulipa kwa kukosa kumbukumbu namba au control number ama wakitaka kulipa control number inakuwa haitambuliki. Serikali tumeboresha mfumo, sasa kumbukumbu namba itapatikana ndani ya dakika moja.” Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply