The House of Favourite Newspapers

Diamond: WCB Tumelipwa Bilioni 2 Kusambaziwa Kazi Zetu na Albamu Yangu Mpya Wamo Rihanna, Rick Ross

diomond-2

STAA wa Bongo Fleva kutoka kundi la WCB, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ leo ameweka bayana kuwa WCB wamesaini kanadarasi kubwa na lebo ya Universal Music Group ili kuwasambazia nyimbo zao duniani kote.

Diamond akiongea katika kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds Fm amesema kuwa lebo hiyo imewalipa dola milioni 1 zaidi ya shilingi bilioni mbili za Kitanzania kuwasambazia kazi zao.

rihanna

Mbali na dili hilo, staa huyo aliyeshirikishwa katika ngoma mpya iliyoachiwa jana na msanii mwenzake wa WCB, Rich Mavoko iitwayo Kokoro amesema anatarajia kuachia albamu ya kimataifa itakayokuwa na kolabo kubwa na za maana.

Rick Ross Mastermind Press photo 2014

Katika albamu yake hiyo ambayo hajasema itatoka lini, Diamond amesema amemshirikisha mwanamuziki Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’ pamoja na William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’ hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula.

Comments are closed.