The House of Favourite Newspapers

Mchungaji Atoa Pepo Kwa Kuwapulizia Waumini Dawa ya Mbu Usoni

doom-south-africa-priest-1

Mchungani mmoja nchini Afrika Kusini amekuwa akiwapulizia usoni waumini wake dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom kwa imani kuwa anawaondolea mapepo na laana walizonazo kwenye maisha yao.

Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, mchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.

Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu, huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko.

doom-south-africa-priest-3Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho na kusema kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.

Nchi hiyo imekuwa na wimbila visa ambapo wajumbe wa kanisawamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili kupata tiba.

Katika picha zilizosambazwa kwenye kurasa za Facebook na Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mountzion General Assembly katika jimbo la Limpopo, anaeonekana akimpulizia dawa ya kuuwawadudu moja kwa moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya mwili mbele ya waumini wa kanisa lake.

doom-south-africa-priest-2‘Nguvu za Mungu’

Amemueleza mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa mmoja wa wanawake kwasababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa “yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu”.

Pia alidai kuwa dawa hiyo ya Doom inaweza kuponesha saratani na virusi vya HIV vinavyosababisha.

Kampuni inayotengeneza dawa ya Doom kwa nembo ya Tiger inasema kuwa inamsihi s mchungaji aliyejitangazia kuwa ”nabii” huko Limpopo – Lethebo Rabalogo kuacha kuwapuliza dawa ya wadudu kwenye nyuso za binadamu kama sehemu ya imani ya kuabudu:

”Tunaona tendo hili kuwa kutia hofu kubwa , na tungependa kubainisha wazi kwamba ni hatari kupulizia Doom ama dawa nyingine yoyote ile ya wadudu kwenye macho ya watu”.

”Doom ilitengenezwa kwa ajili ya kuwauwa wadudu wa aina fulani ambao wameonyeshwa kwenye kopo, na maelezo yaliyoandikwa bayana kwenye kopo la Doom yameonya juu hatari na yanapaswa kufuatwa.”

”Kampuni ya Tiger iko katika mchakato wa kuwasiliana na Nabii kumtaka aache kufanya tendo hilo,” imesema kampuni ya Tiger.

Comments are closed.