The House of Favourite Newspapers

DIAMOND , WIZKID ‘WAVALIANA VIATU ’

Image result for diamond na dyilan

MSANII maarufu wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni msanii aliyevuma sana kutokana na skendo mbalimbali za ngono sambamba na kupata watoto na wanawake wawili tofauti, Zarinah Hassan ‘Zari’ na mwanamitindo Hamisa Mobeto.  Siku za hivi karibuni jamaa alikuwa akivuma sana baada ya kumsaliti mzazi mwenzake Zari, kwani ndio uhusiano uliokuwa ukikubalika na kuheshimika kwa jamii huku Mobeto akiwa ni mpenzi wa siri.

Diamond na msanii Ayodeji Ibrahim Balogun ‘WizKid’ kutoka Nigeria wanavaliana viatu kwani linapokuja suala la kuzaa na wanawake tofauti kisha kuzinguana, wote wapo kwenye kapu moja. Wizkid naye kazaa na wanawake wawili tofauti; Shola Ogudu na Binta Diallo ingawa kwa sasa kajiweka kimapenzi kwa meneja wake, Jada Pollock ambaye naye amezaa naye mtoto mmoja.Image result for diamond baby mama

Wanawake hawa wawili, Shila na Binta ndio wanaoongoza mashambulizi kwenye mitandao ya kijamii kwa kumtusi Wizkid huku wakieleza kuwa, amekuwa hatoi matunzo kwa watoto wao kwani anabagua watoto. Eti anaonekana kumpenda sana mwanaye aitwaye Zion ambaye amezaa na meneja wake.Image result for diamond baby mama

Utakumbuka Diamond naye amewahi kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii kwa tabia yake ya kuwabagua watoto ambapo alionekana kuwathamini sana watoto wa Zari, hayo yalisemwa kabla ya Diamond kuamua kupiga picha akiwa na mtoto wa Hamisa.Image result for wizkid baby mama shola

Wizkid na wanawake wake

Wizkid alikutana na wanawake aliozaa nao kwa nyakati tofauti. Alianza kuzaa na Shola Ogudu aliyekuwa na miaka 19 baada ya kukutana mwaka 2010. Mwaka 2011 wakazaa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Boluwatife. Baadaye Wiz akakutana tena na Video Vixen Binta Diallo, naye mwaka 2016 akamdunga mimba na kupata mtoto wa kiume tena anayeitwa Ayodeji.

Wakati akiwa ameshazaa na wanawake wawili, mshikaji huyo akajikuta tena anampenda meneja wake, Jada Pollock. Baada ya ku-date naye siku kadhaa, ndipo mwaka 2017 wakapata mtoto na hapo ndipo ulipotokea mvurugano.Image result for wizkid baby mama shola

Wote haziivi na waliozaa nao

Wizkid sasa hivi amebaki kuwa na mahusiano mazuri na mwanamke mmoja aliyezaa naye ambaye ni prodyuza wake, waliobaki wawili hapatani nao, kwani kutwa kucha wanamtukana mitandaoni na kutishia kuweka siri zake zote hadharani. “Nimechoshwa na mambo ya huyu mwanaume ambaye hana adabu kabisa, sitaendelea kukaa kimya nitaongea yote yanayomhusu,” aliandika mmoja wa wazazi hao wa Wizkid, Shola Ogudu.

Diamond naye aliwahi kukutana na maneno ya kadhia kutoka kwa wazazi wenzake ambapo amewahi kuambiwa kuwa ni mwanaume ambaye anadhalilisha wanawake, lakini pia amewahi kuambiwa na Hamisa kwamba anasikiliza sana familia yake na maneno mengine ya kashfa baada ya kugombana.Image result for wizkid baby mama shola

Wana umri sawa

Diamond na Wizkid wanalingana kiumri (miaka 28) ni wasanii wanaopendwa Afrika na matukio yao yamerandana, wameweza kutikisa kwa nyimbo zao kwa umri huo mdogo na ndio maana wamekuwa ni kivutio kikubwa kwa wanawake.

Idadi sawa ya watoto

Diamond amebahatika kupata watoto watatu, Latiffa ‘Tiffa’, Nillan na Dylan huku WizKid naye akiwa nao watoto watatu ambao ni Zion, Boluwatife na Ayodeji.

Comments are closed.