The House of Favourite Newspapers

JPM: BALOZI ANAKUNYWA WINE TU, UKITUMBULIWA USILAUMU – VIDEO

RAIS  John Magufuli amewatahadharisha mabalozi wa Tanzania walio nchi za nje kwamba watapoteza nafasi zao ikiwa hawatazitumia  kuleta tija kwa nchi hii.

 

Magufuli aliyasema hayo leo Septemba 29, 2018 baada ya kumwapisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Damas Ndumbaro, leo Ikulu ambapo  alitumia fursa hiyo kumtaka kwenda kuyafanyia kazi mapungufu mengi yaliyomo katika wizara hiyo.

 

Katika hotuba yake fupi katika hafla hiyo, Rais Magufuli alisema amefanya mabadiliko katika wizara hiyo kutokana na mapungufu mengi yakiwemo ya watendaji wake wengi kusahau majukumu hao. Mabadiliko aliyoyafanya ni pamoja na kumwondoa Naibu Waziri na Katibu Mkuu.

 

“Kuna watu  wanadhani walianzia kazi Wizara ya Mambo ya Nje na watastaafia hapo… Unaweza ukatoka wizara yoyote ukafanya kazi foreign (wizara ya mambo ya nje)  au ukapelekwa kuwa balozi ukatuwakilisha. Kama kuna wakurugenzi wanakwamisha hapo ukawatoe, safisha!” alisisitiza Magufuli.

 

Akionyesha msisitizo wa ujumbe wake alisema amekwishawaagiza mabalozi walioko nje kila mmoja alete ripoti inayoonyesha ameisaidia nini Tanzania akiwa huko na “kama kuna balozi atakwenda kule kunywa wine tu, nusu mwaka na hakuna alichofanya, ajiandae kurudi, hafai katika uongozi wangu,” alisema Rais Magufuli.

VIDEO: MSIKIE HAPA JPM AKIFUNGUKA

Comments are closed.