The House of Favourite Newspapers

Diana: Sitaki Tena Maisha ya Bongo Movies

0

MWIGIZAJI wa kike kunako Bongo Movies ambaye kwa sasa amehamishia maskani yake nchini Marekani, Diana Kimari anasema kuwa, anamshukuru Mungu maisha yake ya Bongo Movies ameyasahau na hayataki tena.

 

Katika mazungumzo na Gazeti la IJUMAA kwa njia ya simu, Diana anasema kuwa, hakuna maisha yanayopumbaza kama kuishi Kibongo-Muvi maana hakuna mambo yanayoendelea zaidi ya kujiona wewe zaidi na mambo mengine mengi bila sababu ya msingi, lakini kwa sasa maisha yake yapo tofauti tangu aamie Marekani.

 

“Maisha yangu ni tofauti na huwezi kulinganisha na kitu chochote kile kwa sasa maana ukiishi katika maishaya Kibongo-Muvi, mambo yanaenda ndivyo sivyo ndiyo maanasiyataki tena, lakini sasa mimi ni Diana mwingine na maisha mengine kabisa,” anasema Diana ambaye aliondoka Bongo miaka kadhaa iliyopita.

FULL VIDEO: HARMONIZE KAFUNGUKA YOTE KUHUSU DIAMOND, AVUJISHA SAUTI YA RAYVANNY – “WALISEMA NAROGA”

Leave A Reply