The House of Favourite Newspapers

Diarra, Metacha Matumaini Kibao Yanga Wanampa Furaha Gamondi

0
Makipa wakiwa watatu ambao ni Djigui Diarra raia wa Mali, sambamba na Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia wa Argentina, anatajwa kuwa kwenye furaha kuwaona makipa watatu wakiwa kwenye uimara mazoezini.

Kikosi cha Yanga mpaka sasa kina jumla ya wachezaji 27, huku makipa wakiwa watatu ambao ni Djigui Diarra raia wa Mali, sambamba na Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery ambao ni wazawa.

Taarifa kutoka Yanga, zimeeleza kuwa, makipa wote hao wanampa furaha Gamondi kambini kutokana na kuwa makini kutimiza majukumu yao.

“Kocha anafurahia uwepo wa makipa wetu mazoezini kwa namna wanavyotimiza majukumu yao, anaamini wote wakiwa imara ni mwendelezo wa kuchagua nani ataanza kwenye kikosi cha kwanza,” ilieleza taarifa hiyo.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa, kila mchezaji ndani ya Yanga yupo tayari kwa majukumu yake.

“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kutimiza majukumu, hivyo tunaamini kwamba tutafanya vizuri kwenye mashindano tutakayoshiriki,” alisema.

CHEKI MASHABIKI wa SIMBA SIMIYU WALICHOMFANYIA MCHEZAJI wa ZAMANI wa SIMBA MICHAEL PAUL…

Leave A Reply