The House of Favourite Newspapers

DIDA: HABARI ZA NDOA TUPA KULE

Khadija Shahibu ‘Dida’

LICHA ya kusifika kwa kuwa na bahati ya kuolewa mara nyingi, mtangazaji maarufu wa Redio Times, Khadija Shahibu ‘Dida’ amefunguka kuwa hataki kusikia kitu kinachoitwa ndoa kwani anaona kama inamuongezea maradhi ya vidonda vya tumbo hivyo ni bora ajikite kwenye kutafuta fedha zaidi.  Akizungumza na Za Motomoto News, Dida alisema ameamua kuachana na habari za ndoa licha ya kwamba alivishwa pete ya uchumba lakini aliamua kumwagana na jamaa wake huyo akidai dunia ya sasa siyo ya kuolewa tena.

“Kwa sasa ukiniambia habari za ndoa kwa kweli sikuelewi kabisa maana sitaki vidonda vya tumbo na presha, akili yangu inawaza kutafuta fedha na jinsi ya kumsomesha mwanangu afike mbali aje anitunze mambo mengine nimetupa kule,” alisema Dida.

Dida amewahi kuingia kwenye ndoa mara tatu na zote zikavunjika lakini mwaka jana alivishwa tena pete ya uchumba na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ukuni, Bagamoyo, Issa Seleman lakini uchumba huo uliyeyuka.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.