The House of Favourite Newspapers

Director Kenny, Infinix Tanzania Kuja Kuthibitisha Ubora wa Zero 30 Camera Kwa Vloga

0

Huenda habari kuhusu Infinix ZERO 30 sio mpya masikioni mwako tangu kuzinduliwa kwake imekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii na blog za maswala ya tech. Zero 30 inatajwa kuwa simu ya kwanza ulimwenguni kuja na selfie Camera ya Megapixel 50 yenye uwezo wa kurecord video kwa mfumo wa 4K 60fps kuuzika kwa gharama nafuu zaidi katika masoko ya simu.

Taarifa kutoka @infinixmobiletz simu hii kuja kuuzwa kwa kiasi cha bei za kitanzania Tsh. 1,060,000 tu katika maduka yote ya simu nchini. Miongoni mwa mabadiliko ambayo yamefanyika katika toleo hili la ZERO kupitia ingizo la ZERO 30 ni pamoja na ongezeko la Refresh rate kutoka 120Hz hadi kufikia 144Hz, uchezaji games, uangaliaji na uchukuaji video.

Simu hii pia inakuja na muundo wa 3D yani kioo kinakuwa kimeinama pembezoni kama ambavyo tunaona simu za matoleo ya Samsung S23 na sifa nyingine zimeendelea kutajwa @infinixmobiletz ni kioo aina ya AMOLED, Network 5G na kamera 3 nyuma.

Kwa habari nyepesinyepesi uzinduzi wa simu hii kufanyika kiaina yake tayari kampuni hii imewafikia watengeneza content kupitia camera pamoja na wanahabari ili kuonyesha uhalisiawa ZERO 30 katika kurecord video kupitia camera ya mbele.

Moja ya mchukua content mashuhuri nchini ambaye atakuwepo katika uzinduzi huo unaotegemewa kufanyika Tarehe 26 ya Mwezi huu wa Septemba ni pamoa na Director Kenny @director_kenny ambaye anafanyakazi nyingi za wasanii mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Tembelea @infinixmobiletz au maduka yao ya simu kufahamu zaidi kuhusu Infinix ZERO 30 au piga 0659987284.

Leave A Reply