The House of Favourite Newspapers

Kampuni ya Ziiki Media Yamkana Diamond, Yasisitiza Siyo Mmiliki Wala Hana Hisa

0

 

Baada ya uvumi wa muda mrefu kwamba staa wa Bongofleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ndiye mmiliki wa Kampuni ya Usambazaji wa Muziki ya Ziiki Media, Meneja wa kampuni hiyo, Camilla Owora ametoa ufafanuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Camilla amekanusha uvumi huo na kueleza kuwa Diamond siyo mmiliki, siyo mwekezahi wala hana hisa zozote Ziiki Media.

 

Amesisitiza kuwa Ziiki Media haijawahi kuwa na ubia wa aina yoyote na Diamond zaidi ya kuingia naye mikataba ya kusambaza kazi zake na za wasanii waliopo chini ya lebo yake WCB.

Leave A Reply