The House of Favourite Newspapers

Diwani, Dereva Halmashauri ya Meatu Wafariki Ajalini Singida

DIWANI wa Kata ya Manuzi, Elias Shukia,  na dereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Haruna Ngata,  wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka mara tatu.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu,  amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mkiwa, wilayani Singida.

Ameongeza kuwa Mkuregenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manuzi na  mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Pius Machungwa,  na watu wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambapo majeruhi wanne wamelazwa  hospitali ya St Gasper iliyopo Itigi na wawili wamelazwa hospitali ya Puma wilayani Ikungi.

“Chanzo tulichokiona kwenye eneo la tukio ni kupasuka kwa tairi la mbele kushoto.  Hata hivyo,  tuwasubiri polisi wafanye uchunguzi zaidi  kuhusu chanzo halisi cha ajali yenyewe,” amesema.

Comments are closed.