The House of Favourite Newspapers

WAHITIMU SM ILALA BOMA 2000 WAKARABATI DARASA

Ofisa Elimu,  Vifaa na Takwimu Wilaya ya Ilala  kwa niaba ya mkurugenzi wa wilaya hiyo, Asha Mapunda, akikata utepe kupokea chumba cha darasa kilichokarabatiwa na wahitimu wa shule hiyo mwaka 2000.
Hafla ya kukata utepe ikiendelea. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Adrian Kabopile (kushoto), Mapunda, na mhitimu wa mwaka 2000 ambaye ndiye mratibu Group la WhatsApp, Hawa Barongo.
Mhitimu wa mwaka 2,000 ambaye ndiye mratibu wa Group la WhatsApp, Hawa Barongo (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkoani Wilaya ya Ilala wakifutailia kilichokuwa kikiendelea.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Mkoani na wahitimu wa mwaka 2000.
Picha ya pamoja.
Keki maalum iliyoandaliwa katika hafla hiyo.

 

 

 

WANAFUNZI waliowahi kusoma Shule ya Msingi Boma Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,  ambayo sasa inaitwa Shule ya Msingi Mkoani, wamekarabati darasa moja kwa lengo la kurudisha  fadhila walizozipata wakiwa wanasoma hapo kwa kuwa ndiyo umekuwa msingi bora wa mafanikio ya wanafunzi wengi waliosoma katika shule hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya hiyo,  mgeni rasmi ambaye alikuwa  Ofisa Elimu,  Vifaa na Takwimu Wilaya ya Ilala,   kwa niaba ya mkurugenzi wa wilaya hiyo, Asha Mapunda, aliwapongeza wanafunzi hao kwa umoja wao na fadhila kwa kukumbuka shule waliyosoma akisema  serikali haiwezi kufanya kila jambo,  hivyo wadau mbalimbali ni msingi katika kuhakikisha maendeleo ya shule yanasonga mbele.

 

 

Kwa upande wake, mhitimu wa mwaka 2,000 ambaye ndiye mratibu Group la WhatsApp, Hawa Barongo,  amesema kuwa lengo ni kurudisha fadhila kwa walimu wao na hata kwa jamii kwa ujumla huku akisema hawatachoka kuhakikisha kila wakati wanatafuta pesa za kusaidia kukarabati shule hiyo kutokana na miundombinu ya zamani kuwa si rafiki kwa wanafunzi.

 

 

“Maendeleo niliyopata mimi ni kutokana na kupata elimu katika shule ya Ilala Boma hivyo lazima tuikumbuke kwa kuendelea kuipatia msaada kadiri tunavyoweza maana ukituangalia hapa unatuona wote tuna vipato vizuri hivyo ni budi kukumbuka wapi tumetoka na tulikotoka kupoje, hivyo tutaithimini hii shule kila wakati kama tulivyofanya hivi sasa” alisema Hawa na kuongeza kuwa:

 

 

“Leo tumerudi katika shule hii inayoitwa hivi sasa Shule ya Msingi Mkoani kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii ukizingatia kuwa shule hii ina uchakavu wa majengo na miundombinu,  hivyo sisi  tumeanza kwa kukarabati darasa hili ambalo lilikuwa halina sakafu na tumepaka rangi ndani ya darasa hili lakini changamoto bado zipo nyingi hivyo hatutachoka kusaidia shule yetu hii, tutaendelea.”

 

Hawa amewataka wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule hiyo kurudisha upendo katika shule hiyo kwa kuwa ndiyo chanzo cha mafanikio yao ya sasa.

 

Mwalimu Mkuu wa shule  hiyo, Jane Mganwa,  amewapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa upendo wa kujitoa kwa ajili ya wadogo zao ili waweze kusomea kwenye madarasa yaliyo bora.

 

Comments are closed.