The House of Favourite Newspapers

TANZIA: DJ Juice Hatunaye, Azikwa Dar

0
Mchezeshaji maarufu wa muziki nchini,Hussein Juma Amani Misana ‘DJ Juice’.

Msiba! Mchezeshaji maarufu wa muziki nchini, DJ Juice ambaye jina lake halisi ni Hussein Juma Amani Misana, amefariki dunia juzi.

Kwa mujibu wa kaka yake, Amani Misana, DJ Juice alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu na juzi jioni alizidiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, lakini akafariki njiani.

Wadau mbalimbali wakiwa katika mazishi ya Dj Juice katika makaburi ya Ndumbi, Magomeni jijini Dar.

“Marehemu alikuwa anasumbuliwa na TB, ilikuwa ina kama siku tano na alikuwa anatumia dawa, sasa juzi jioni akazidiwa, tukamkimbiza Lugalo, lakini tulipofika Mwenge Mataa, akafariki,” alisema Misana, ambaye pia ni mtangazaji maarufu wa redio.

Marehemu ambaye pia amepata kuwa DJ wa ukumbi maarufu wa Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem, ameacha mke na watoto watatu.

Mazishi yake yamefanyika jana katika Makaburi ya Ndugumbi yaliyoko Magomeni jijini Dar.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina!

Na Mwandishi Wetu|DAR ES SALAAM

Leave A Reply