The House of Favourite Newspapers

DJ KHALED AWABURUZA MAHAKAMANI BILLBOARD


MUANDAAJI wa muziki nchini Marekani, DJ Khaled, ametumia kiasi cha ($5 million) sawa na TZS Bilioni 11 kuandaa album yake ya Father Of Asahd.

Hata hivyo, huenda atawapeleka mahakamani Billboard kwa kuwa album yake imeshindwa kukamata namba moja kwenye chati za Billboard 200 wiki moja baada ya kuachiwa rasmi.

Khaled ameamua kuipeleka kortini Billboard ni kwa sababu ya kushindwa kuchukua mahesabu (100,000 Units) ya mauzo ya nguo “Merch” za album hiyo kama walivyofanya kwa “IGOR” ya Taylor The Creator ambayo ilikamata namba moja.

Billboard wana hesabu na mauzo ya bidhaa za nguo (Merchandise Sales) na huyaweka kwenye mjumuisho wa mauzo ya nakala za album. Tukio hili linakumbusha  mtafaruku wa aina hii baina ya Nicki Minaj (QUEEN) na Travis Scott (AstroWorld) mwaka jana!

Comments are closed.