The House of Favourite Newspapers

Dj Sinyorita Alamba Shavu Baada ya Kuchaguliwa Kuwa Balozi wa Kampuni ya ORAIMO

0

 

 

Dj wa kike aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kucheza na mashine, Dj Sinyorita amelamba shavu la nguvu baada ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Kampuni ya ORAIMO inayoongoza Afrika kwa kuuza ‘accessories’ zenye ubora wa hali ya juu.

WIki iliyopita, kupitia akaunti yake ya Instagram, Dj Sinyorita aliwauliza mashabiki wake akisema: “Naombeni mnitagie ‘the best earpod’ kali hapa ili nipange playlist noma kwa ajili yenu.”

Post hii ikasababisha Kampuni ya ORAIMO kupendekeza earpod zao mpya za FREEPOD 4 ambapo baada ya kushangazwa na ubora wake, kampuni hiyo ikaamua kumpa ubalozi Dj huyo kwa ajili ya kutangaza eapods hizo na kualikwa katika uzinduzi rasmi wa bidhaa hizo.

Uzinduzi wa FREEPOD 4 ulifanyika Ijumaa ya Machi 3, 2023 ambapo DJ sinyorita alihudhuria kama mgeni rasmi lakini pia alipata nafasi ya kuwaambia wapenzi wa bidhaa za ORAIMO kuwa FREEPOD 4 ni tofauti na earpod alizokuwa anatumia zamani maana amevutiwa na design yake (SLIDE CASE), mdundo na betri inayodumu zaidi ya saa 35 ambapo pia ni rahisi kuzitumia maana kuna APP special kwa ajili ya kuzicontrol earpods zako na sifa nyengine kibao.

FREEPOD 4 Ni bidhaa mpya kutoka kampuni ya accessories ORAIMO ambayo imeboreshwa zaidi kwenye upande wa betri ambapo utaweza kusikiliza muziki mzuri kwa zaidi ya saa 30.

Sio hivyo tu bali inakuja na sifa nyingine ya Active Noise Cancellation ambayo inakusaidia kusikiliza muziki au kuongea na simu bila muingiliano wa sauti za nje.

FREEPOD 4 inazuia sauti za nje ambapo hautaweza kusikia sauti za watu au vitu vingine pindi ukiweka ON na itakupa uhuru wa kuenjoy kila utakachokuwa unasikiliza.

Pia Kwa wale watumiaji na wapenzi wa Earbuds, hii bidhaa ni special kwao maana inakuja na muundo mpya wa Sliding Case pamoja na APP rasmi (oraimo sound) utakayotumia kuzi-control buds zako. Pia wameboresha zaidi Betri, Muonekano na Functions zitakazopatikana ndani ya App.

Bidhaa hii inapatikana katika maduka yote ya Accessories Tanzania nzima. Hivyo basi wapenda bidhaa za ORAIMO au wapenzi wa kutumia Earbud mjiandae kupokea bidhaa hii kali.  Kufahamu Zaidi kuhusu bidhaa za ORAIMO tembelea tovuti yao: https://www.oraimo.com/.  Au kwenye page zao za mitandao ya ijamii : https://www.instagram.com/oraimotz/

 

Leave A Reply