The House of Favourite Newspapers

Dkt. Kigwangalla Afanya Ziara ya Kushtukiza Foreplan Clinic ya Dkt. Mwaka

0

DSC_0004

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwasili katika kituo cha Foreplan Clinic kinachotoa tiba mbadala kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho jana jioni. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na Tiba Mbadala Dk.Paul Mhame wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

DSC_0013Dkt. Kigwangalla akipokelewa na mmoja wa wauguzi wa kituo hicho ambapo jina lake halikupatikana kwa haraka baada ya Mkurugenzi wa kituo hicho Dk. Mwaka Juma Mwaka kutokuwepo kwenye kituo chake cha Foreplan Clinic kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam.
DSC_0025DSC_0035Dkt. Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wananchi waliofika kupata matibabu katika kituo cha Foreplan Clinic kuhusu huduma zitolewazo katika kituo hicho kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka.DSC_0043Msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya akimtolea ufafanuzi Dkt. Kigwangalla kuhusu huduma zitolewazo katika kituo cha Foreplan Clinic mara baada ya kuanza kukagua kituo hicho kinachotoa tiba mbadala.DSC_0059Dkt. Kigwangalla akikikagua kifaa kinachotumika kufanyia vipimo kwenye kituo cha Foreplan Clinic wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho jana jioni Desemba 14, 2015.DSC_0060Hiki ndicho kifaa kinachotumika kupimia wagonjwa kwenye maabara ya kituo hicho cha tiba mbadala.DSC_0069Dkt. Kigwangalla akiwauliza maswali wasaizizi wa kituo hicho wakiongozwa na Bi Teddy L. Mbuya mara baada ya kukuta hali ya sintofahamu katika kituo hicho.DSC_0086Dkt. Kigwangalla akikagua moja ya dawa zinazotolewa kwa wangonjwa wanaokuja kutibiwa kwatika kituohicho cha tiba mbadala.DSC_0089Bi. Rozaria Anthony ambaye ni muhudumu wa dawa akikaa kimya baada ya kuulizwa maswali na Dkt. Kigwangalla na kukosa la kujibu.DSC_0097Hizi ni dawa za asili zinazouzwa katika kituo hicho cha tiba mbadala.DSC_0104Dkt. Kigwangalla akimpa maelekezo Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala jana majira ya jioni amefanyaziara ya kushtukiza katika kituo kinachotoa tiba mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya kituo hicho.

Mara baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu ya Mapokezi mpaka kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote hakuna daktari aliyekuwa anatoa huduma.

Akizungumza na wagonjwa waliokuwa wakisubiria tiba alisema kuna waliofika katika kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa hao.

Na kuwataka wagonjwa hao waende kwenye hospitali ili wapate matibabu yanayoendana na magonjwa wanayoumwa.

Akizungumza msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji mkuu bali alimwomba Naibu Waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho pamoja na kuwauliza maswali wahusika mbalimbali wa vitengo vya kituo hicho.

Baada ya ukaguzi wa kituo hicho Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na Mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya ukaguzi kwa kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika kuhusu taaluma yeke pamoja na washirika wake na pia dawa anazozitumia kama ni rafiki kwa wananchi wanaotumia dawa hizo pamoja na kufanya ukaguzi wa vituo vyote vinavyotoa tiba mbadala na tiba asilia kama Dk. Ndodi, Dk. Rahabu nk. ili kuwabaini wanaowalaghai wananchi.

Pia amesema Dk. Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo mbalimbali hapa nchini ambavyo ni kosa la kutangaza kama unafanya kazi za tiba tabibu.

Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo inatumika na mojawapo ikiwa ni kutojitangaza.

Naibu waziri aliendelea kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na amekuwa akichambua mwili wa binadamu kama vile ameusomea udaktari wakati sheria ya tiba asilia na tiba mbadala hairuhusu watu wa tiba asilia na Tiba mbadala kutumia maneno ya tiba ya kisasa.

Pia Naibu Waziri amemtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani leo saa mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.

(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)

Leave A Reply