The House of Favourite Newspapers

Dkt. Abbas: Ahadi ya Rais Tayari, Mfuko wa Sanaa Umehuishwa

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara hiyo imekwishatekekeza Ahadi ya Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhuisha Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni.

 

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Desemba Mosi jijini Dar es Salaam jioni hii katika mwendelezo wa ziara yake katika tasnia ya sanaa nchini na amewataka wasanii wa muziki wa kizazi kipya aliokutaka nao leo kuwasilisha mahitaji ya mafunzo ndani ya siku 30 ili utaratibu uanze.

 

“Tumetekeleza Ahadi Mfuko upo na Bodi yake ipo tunasubiri kuizindua tu kama alivyosema Mhe Rais wakati wa kampeni zake Mfuko huu utatoa mikopo na mafunzo kwa wasanii na wanatasnia za utamaduni nchini na tuanze kuwasilisha mahitaji hasa eneo la mafunzo tuboreshe kazi zetu,” alisema Dkt. Abbasi

Kesho katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu huyo atakutana na wasanii wa Bongo Movie.

Leave A Reply