The House of Favourite Newspapers

Mastaa Wamezea Mate Penzi la Vanessa

0

MASTAA wengi Bongo wamekuwa wakieleza waziwazi wanavyoizimikia na kuimezea mate kapo ya staa mwenzao wa
kike Bongo, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na mpenzi wake, Olurotimi Akinosho almaarufu Rotimi.

Rotimi ni staa wa muziki, uigizaji na mitindo mwenye asili ya nchini Nigeria aliyezaliwa huko Maplewood, New Jersey nchini Marekani.

Penzi la wawili hao limezidi kutaradadi siku hadi siku kiasi cha wawili hao kujichora tatuu za majina yao kweye vifua vyao, kapo ya Vanessa na Rotimi inatajwa kuwa miongoni mwa pea za wapenzi wenye furaha zaidi kutokana na kila siku kuonekana wakijiachia na kuoneshana mahaba kama yote.

Picha za Vanessa na Rotimi zimekuwa zikisambaa mitandaoni wakiwa viwanja tofauti ambapo wenyewe, wanaoneshana mahaba ya aina yake.

Baadhi ya mashabiki wao wakiwemo mastaa lukuki wa Bongo wamekuwa wakiwasifi a na kuwapongeza kwa namna ambayo hawafi chi furaha ya penzi lao. Baadhi ya wasanii wamekuwa wakitamka waziwazi kuwa wanatamani kuwa kwenye mapenzi ya aina hiyo.

 

Wengi wamejikuta wakishindwa kujizuia na kuangusha komenti za aina yake kwenye ukurasa wa Instagram wa
Vanessa huku wakimuuliza sehemu aliponyeza ili na wao wapate wapenzi wenye mahaba kama yak wake na Rotimi.
Wengine wamekuwa wakimuombea mwanadada huyo heri na baraka tele kwenye penzi lako hilo.
Kama ulikuwa unategemea kuna siku

Vanessa na Rotimi wataachana, basi sahau hilo kwani wenyewe wameapa kutoachana. Kauli hiyo ilitolewa na Rotimi mara baada ya kutokea katika kipande cha video ambayo Vanessa aliiweka katika ukurasa wake wa Instagram akijibu swali la kwa nini yupo kimya huku sababu kubwa ikitajwa ni kutekwa kimapenzi.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply