The House of Favourite Newspapers

Wasanii Wekezeni Kwenye Kazi Bora Si Kiki – Dkt Abbasi

0

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ametoa msimamo kuwa Serikali haitapoteza muda na wasanii wanaoendeleza kiki badala ya kutumia muda wao vizuri kutengeneza kazi zao bora za sanaa.

 

 

Ameyasema hayo Dar es Salaam leo alipokuwa akitembelea eneo la Kivukoni ambapo Serikali inakamilisha taratibu kuziweka katika ofisi moja taasisi za sanaa ambazo ni Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Taasisi ya Hakimiliki (Cosota) na Bodi ya Filamu Tanzania (FBT).

 

 

“Serikali kama alivyoahidi Mheshimiwa Rais ipo kazini kuhakikisha sekta za sanaa zinakua na kuwapatia vijana mchango chanya. Hapa leo tunapambania taasisi zetu hizi muhimu kwa wasanii wapate ofisi nzuri na wawahudumie wasanii kutokea sehemu moja baada ya malalamiko ya miaka mingi kuwa ziko mbalimbali lakini unashangaa baadhi ya wasanii kuwaona siku mbili hizi wanaturudisha nyuma kwenye maisha ya kiki badala ya kazi bora,” alisema Dkt. Abbasi.

 

 

Akizungumzia ziara hiyo ya kukamilisha taratibu za ofisi za pamoja kwa taasisi hizo, Dkt. Abbasi alisema uamuzi umeshapitishwa na sasa ni taasisi hizo kugawiwa na kuhamia eneo moja na kuanza kutoa huduma bora kwa wadau wao kutokea sehemu moja kwa jijini Dar es Salaam wakati mipango kama hiyo ikiendelea kwa makao makuu Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply