The House of Favourite Newspapers

Dkt. Bashiru Amuonya Bernard Membe

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya mwanachama wake ambaye ni waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Bernard Membe, kutokuwa juu ya katiba ya chama hicho.

 

Onyo hilo limetolewa leo tarehe 27 Novemba 2019 na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, wakati akizungumza  na kituo cha televisheni cha ITV cha jijini Dar es Salaam,  ambapo amesema kama Membe ataendelea kutofuata utaratibu, uongozi wa chama hicho utamlazimisha kufuata utaratibu.

 

“Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu. Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine…  Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

 

“Membe hayuko juu ya katiba, Mwalimu Nyerere aliasisi CCM na hakuwa juu ya katiba.  Membe akitaka kuwa mwanachama kama wengine wa CCM, afuate utaratibu, asipofuata mimi ndiye msimamizi wa utaratibu huo atalazimishwa kufuata utaratibu,” alisema.

 

Hata hivyo, amesema Membe hakuwahi kujadiliwa katika vikao vya chama, licha ya kwamba hakuitikia wito wake, alipomtaka kuonana naye akiwa mkoani Geita.

 

“Hatukuwahi kumjadili na kwenye vikao hakuwahi kufika. Kosa halifi kama jinai, kosa halifi unaweza ukadhani limekufa kumbe ni utaratibu wa wakati. Kupitia kwako, naomba kueleza wana CCM tuko makini kulinda utamaduni wa chama, na wanachama kutii viapo vyao,” amesema Dk. Bashiru.

 

“Nimekuja kuimarisha chama na hasa kufunga mitambo ya ushindi mwaka kesho, baada ya majaribio ya mitambo hiyo kufanya kazi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, natembea wilaya zote za Unguja na Pemba nikifunga mitambo,” amesema Bashiru.

Comments are closed.