The House of Favourite Newspapers

Dkt Kigwangalla Adai Dhambi Aliyoifanya Dkt Bashiru Haistahili Huruma

0
Mbunge wa Nzega Vijijini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Hamisi Kigwangalla

MBUNGE wa Nzega Vijijini na aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla ameibuka na kudai kuwa dhambi aliyoifanya Mbunge wa kuteuliwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM dkt Bashiru Ally kwa kudharau, kukejeli, Kunajisi na kudogosha juhudi za Rais kwenye kuboresha maslahi ya wakulima haistahili huruma.

Chapisho la kwanza la Dkt Kigwangalla wakati Dkt Bashiru anateuliwa kuwa Mbunge na kuondolewa kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)

Dkt Kigwangalla ametoa maneno hayo kupitia chapisho lake aliloandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ikiwa ni sehemu ya kuonesha kutomuunga mkono Dkt Bashiru kuhusu kauli yake juu ya juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan na utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi.

Andiko la Dkt Kigwangalla baada ya kauli ya Mbunge wa kuteuliwa Dkt Bashiru juu ya kukejeli juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwa wakulima.

Ikumbukwe awali wakati Dkt Bashiru anateuliwa kuwa Mbunge na kuachia wadhifa wake wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tukio hilo lilipokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wadau wa siasa na wananchi baadhi wakimcheka na kumkejeli lakini kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter Dkt Kigwangalla aliandika na kumkingia kifua Dkt Bashiru akiamini hatua ile ilikuwa ni riziki mpya na mipango ya mungu.

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kuteuliwa Dkt Bashiru Ally

Leave A Reply