The House of Favourite Newspapers

Dkt. Mpango Amwagiza Mwigulu ‘Mapato Tril. 2 kwa Mwezi’ – Video

0

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewaagiza Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Muungano na Mazingira, Selemani Jafo kuhakikisha kazi yao ya kwanza ni kutatua changamoto ya kifedha ya Muungano wa Tanzania.

 

 

Dkt. Mpango amesema hayo leo, Alhamisi, Aprili 1, 2021, Ikulu ya Dodoma wakati wa uapisho wa mawaziri nane na manaibu waziri wanane ambapo pia amemwagiza Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa mwaka 2021, wastani wa ukusanyaji mapato ya serikali unafikia TZS trilioni 2.

 

 

“Jana Mhe. Rais Samia Suluhu ulikemea utaratibu wa mawaziri na manaibu Waziri kuvutana, na hili tutalisiamamia. Tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kuvutana, pia kuna mvutano kati ya makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu.

 

 

“Serikali yako wananchi wamepata matumaini makubwa, umeikamata nchi vizuri na kwa haraka. Natamani kufikia mwisho wa mwaka huu (2021), makusanyo yawe Tsh trilioni 2 kwa mwezi, na nafikiri inawezekana.

 

 

“Kuna mvutano kati ya mawaziri na naibu mawaziri, hili nitalifuatilia kama alivyosema Rais (Samia Suluhu Hassan), tunajenga nyumba moja kwa nini tuvutane, mawaziri wapeni kazi manaibu wetu. Hili lipo pia kwa katibu na naibu katibu wakuu,” amesema Dkt. Mpango.

Leave A Reply