The House of Favourite Newspapers

Dkt. Senkoro Kuzikwa Jumamosi Jijini Dar

senkoro-2

Marehemu enzi za uhai wake.

senkoro-1

Kaka wa marehemu Senkoro aitwaye George Nathaniel akizungumza na wanahabari kuhusu ratiba ya mazishi na taratibu nzima zinazoendelea nyumbani kwao Tabata Segerea.

senkoro-3

Mtoto wa marehemu aitwaye Joan Japhet akizungumza jambo na vyombo  vya habari.

senkoro-4

Kaka wa marehemu akiendelea kutoa ufafanuzi.

MWILI wa aliyekuwa  mgombea urais wa kike wa kwanza nchini katika uchaguzi  mkuu wa 2005 kupitia chama cha APPT-Maendeleo, Dkt. Anna Claudia Senkoro, aliyefariki dunia jana, unatarajiwa kuzikwa Jumamosi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

senkoro-5

Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu .

Taarifa kutoka kwa kaka wa marehemu,George Nathaniel,akizungumza na mtandao huo alisema  mwili wa marehemu unatarajiwa kutolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili siku ya Jumamosi na kupelekwa nyumbani kwake Tabata Segerea-Mzimuni  kabla ya kupelekwa kanisa la  Winner Chapel International  lililopo Ukonga, Dar kwa ajili ya ibaada na utoaji wa heshma za mwisho.

senkoro-6

Aliyekuwa Mbunge wa Segerea, Makongoro Mahanga, akielezea wasifu wa marehemu.

Baada ya hapo mwili utaelekea katika nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kinondoni majira ya mchana kwa ajili ya maziko.

senkoro-7

Taswira ya nyumbani kwa marehemuSenkoro huko Tabata Segerea-Mzimuni.

Marehemu alishiriki uchaguzi wa mwaka 2005 uliomuingiza madarakani Jakaya Kikwete ambapo marehemu alishika nafasi ya nane kwa wingi wa kura na kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwania nafasi hiyo toka Tanzania Bara ipate uhuru.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.