The House of Favourite Newspapers

Kiwanda cha takataka kujengwa Kinondoni

meya-sitta-1

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Samwel Sitta akisaini kwenye kitabu cha wageni cha Ofisi za Global Publishers alipofika kufanya mahojiano na Global TV Online. Kulia ni Mhariri Kiongozi, Oscar Ndauka.

meya-sitta-2

Benjamin Sitta akifanya mahojiano na Global TV Online.

meya-sitta-3

…Akijibu swali.

meya-sitta-4

meya-sitta-5

…Akifafanua jambo

meya-sitta-6

Benjamin Sitta (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mhariri wa gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul (kushoto) pamoja na Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli, baada ya mahojiano,

Na Elvan Stambuli

MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Samwel Sitta amesema manispaa yake itajenga kiwanda cha kuchakata takataka na kutoa ajira ya zaidi ya watu 500 mwaka huu.

meya-sitta-7

Sitta akizungumza na wahariri baada ya mahojiano.

Akifanya mahojiano na Global TV Online katika Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga Mwenge Dar leo, Meya Sitta alisema mchakato wa kupata kiwanda hicho umekamilika na kinafadhiliwa na Wajerumani wa Mji wa Humburg.

meya-sitta-8

Akiagana na Viongozi wa Global Publishers.

“Takataka zitakuwa ni fedha kama zilivyo chupa za plastiki. Kutakuwa na magari ambayo yatakuwa yakikusanya takataka mjini na kwenda kuyasindika kuwa mbolea kwenye kiwanda Mabwepande. Kuna faida nyingi za mradi huo kwani mji utakuwa safi na pili vijana watapata ajira,” alisema Meya Sitta.

meya-sitta-9

Alisema licha ya kiwanda hicho, kuna mpango katika manispaa yake kuboresha makazi ya watu kama vile Tandale, Mwananyamala na Uwanja wa Fisi, Manzese ambako kutajengwa maghorofa ya kisasa baada ya makubaliano na wananchi wa maeneo hayo na manispaa yake.

Picha na Musa Mateja/GPL

Comments are closed.