The House of Favourite Newspapers

Dogo Janja: Kama si muziki ningekuwa marehemu!

0

Janjaro2_NoizWIKI hii kwenye safu yetu ya 10 Questions tunaye msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya anayefahamika zaidi kwa jina la Dogo Janja ila jina lake la kuzaliwa ni Abdulaziz Abubakar Chende.

Yuko hapa kujibu maswali aliyoulizwa na Mwandishi wetu Gabriel Ng’osha!

Ijumaa: Umerudi kwa kasi kwenye gemu na sasa unatamba na wimbo wako wa My Life, unaizungumziaje ngoma hiyo?

Dogo Janja: Iko poa sana na kiukweli imenifanya nitambulike kimataifa.

Ijumaa: Unamaanisha nini kusema ngoma hiyo imekufanya utambulike kimataifa?

Dogo Janja: Imevuka boda, imesikilizwa na wasanii wakubwa nje na ndiyo maana nimepata fursa ya kufanya remix ya wimbo huo na wasanii wa Uganda, Radio na Weasel.

Ijumaa: Ilikuaje ukakutana nao?

Dogo Janja: Chameleon aliwaunganisha na menejimenti yangu nikawatumia biti, wakafanya yao na hivi karibuni video yake itawajia.

Ijumaa: Sasa hivi umekuwa mkubwa, hivi shemeji yetu ni nani maana tunakuona upo upo tu?

Dogo Janja: Kiukweli sina na kwa sasa nataka kufanya kazi, mapenzi pembeni kwanza.

Ijumaa: Ni sawa lakini unadhani ni demu wa aina gani ambaye siku za usoni unaweza kumuita mke?

Dogo Janja: Sifa kubwa awe mcha Mungu, mengine yatafuata.

Ijumaa: Hivi inawezekana kuja kutokea ukaingia kwenye maisha ya ndoa na staa mwenzako?

Dogo Janja: Haitatokea, mastaa wana drama nyingi.

Ijumaa: Hivi Dogo Janja kabla ya ustaa ulikuwa ni mtu wa aina gani?

Dogo Janja: Mhuni, mtukutu na mtu wa fujo za ajabuajabu.

Ijumaa: Unahisi ungekuwa wapi kama bado ungekuwa unaendelea na utukutu wako?

Dogo Janja: Dunia isingenifahamu, bila shaka ningekuwa marehemu.

Ijumaa: Kwa nini unasema hivyo?

Dogo Janja: ‘Manyang’au’ wenzangu kibao walishafariki, wengine wemechomwa moto, wengine wamepigwa mawe mpaka kufa kwa sababu ya utukutu, unyang’anyi na matukio kama hayo.

Ijumaa: Nini kinafuata baada ya Wimbo wa My Life?

Dogo Janja: Mashabiki wategemee vitu vya ukweli, nimejipanga kufanya mapinduzi makubwa sana kwenye gemu.

Leave A Reply