The House of Favourite Newspapers

Banana: Mademu wenye swaga za asili wananikosha

0

bananaSTORI: BONIPHACE NGUMIJE

MSANII wa muziki anayefanya poa kwenye gemu la muziki Bongo, Banana Zoro amefunguka kuwa, anavutiwa zaidi na wanawake wenye swaga za asili ya Kiafrika kuliko wanawake wenye swaga za Mamtoni anaowachukulia kuwa wanautupa utamaduni wao.

Akipiga stori na Ebwana Dah, Banana alisema kuwa, suala hilo limemfanya kila mahali anapomuona mwanadada mwenye swaga za kiasilia kujikuta akitamani kuwa naye karibu.

“Nawa-penda na kuwaheshimu sana wanadada wenye swaga za kiasili, mara kwa mara nimekuwa nikipenda sana kuwa karibu yao ndiyo maana hata hivi karibuni tulipomaliza kushuti Video ya Sizonje ya Mrisho Mpoto nilijikuta nikitamani kupiga picha na kila mwanadada aliyetupia kiasili, wanavutia kiukweli kuliko wale wanaovaa kimamtoni zaidi,” alisema Banana.

Leave A Reply