The House of Favourite Newspapers

Don Jazzy Kuja na Tamasha la Mavin Records

0

Mkongwe wa muziki kutoka Naija na mkurugenzi wa Lebo ya Muziki ya MAvin, Don Jazzy.

MKONGWE wa muziki kutoka Naija na mkurugenzi wa Lebo ya Muziki ya MAvin, Don Jazzy anatarajia kuja na tamasha bab’ kubwa la kusherehekea lebo yake, Desemba 23, mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari Nigeria, Don Jazzy alisema wameamua kuandaa tamasha hilo kama shukurani kwa mashabiki wao ambao wamekuwa wakiwaonyesha sapoti tangu mwaka 2012 ilipoanza kujipatia umaarufu zaidi.

“Mipango ya tamasha letu inakwenda vizuri, nachukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wetu wakuu ambao ni Benki ya Access na mashabiki wetu waliotuunga mkono tangu mwaka 2012,” alisema Don Jazzy.

Mavin Records ina vichwa kibao ambavyo vinabamba kunako muziki wa Nigeria na Afrika kwa ujumla ambavyo ni Tiwa Savage, Reekado Banks na Korede Bello.

Leave A Reply