The House of Favourite Newspapers

Donald Trump Kufanya Mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais Donald Trump atazungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hivi karibuni kwa njia ya simu. Mazungumzo yao yatakuwa ya kwanza tangu rais huyo wa Marekani apate ushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Uhuru Kenyatta atakuwa rais wa nne wa Afrika kuzungumza na rais huyo kutoka Marekani, Taifa lenye uwezo mkubwa duniani.

Rais Uhuru Kenyatta.

Kati ya marais wa Afrika aliozungumza nao kwa njia ya simu ni Rais wa Misri Abdel Fatah al Sisi, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari .

Miongoni mwa maswala wanayotarajiwa kugusia ni swala la usalama, Somalia na ukame unaendelea kukumba eneo zima la Afrika Mashariki.

Comments are closed.