The House of Favourite Newspapers

FFU Watumia Nguvu Kutuliza Ghasia Simiyu

Askari wa kutuliza Ghasia FFU akimfukuza mwanafunzi

WANAFUNZI takribani 600 wa Shule ya Sekondari ya Bariadi iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu wameandamana na kufunga Barabara Kuu ya Bariadi- Lamadi kupinga kuhamishwa kwa mkuu wa shule hiyo Dues Toga.

Askari wanne wa kutuliza Ghasia wakimdhibiti mwanafunzi

Wanafunzi hao walianza kuandamana kwenda katika ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri, lakini ilishindikana baada ya kikosi cha jeshi kuzuia ghasia (FFU) kuwazuia kwenda katika ofisi hizo.

Wanafunzi wakiwa barabarani na mabango

 

 

Askari wa FFU wakielekea katika ofisi za shule hiyo
Walimu wakijaribu kuwatuliza wanafunzi
Wanafunzi wakimpa huduma ya kwanza mwanafunzi mwenzao aliyezimia baada ya kulipuliwa kwa mabomu ya machozi
…wakinesha bango kwa wanahabari

Kaimu mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga akipokea bango kutoka kwa wanafunzi

Hata hivyo wanafunzi hao wakiwa katikati ya barabaara hiyo waliamua kuandamana tena kuelekea ofisi za mkuu wa mkoa jambo lililoshindikana baada ya askari hao kuwazuia eneo la hospitali ya teule ya mkoa (Somanda)

 

Kaimu mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga,

 

Comments are closed.