The House of Favourite Newspapers

DRC Kuharakisha Kuondoka kwa Wanajeshi wa UN Nchini Humo

0
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi

SERIKALI ya DRC Congo imesema kuwa inatumai itaharakisha kuwaondoa Wanajeshi wanaolinda Amani wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO nchini humo.

 

Kupitia makubaliano mapya, Wanajeshi hao wa UN walitarajiwa kuondoka mwishoni mwa mwaka 2024.

 

Tangazo la kuwaondoa Wanajeshi hao Linajiri kufuatia maandamano ya ghasia dhidi ya Vikosi hivyo vya UN katika eneo la Mashariki mwa Taifa hilo ambayo yalisababisha Mauaji ya makumi ya Raia pamoja na Wanajeshi Wanne wa UN.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa

Siku ya Jumatatu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres aliomba msamaha baada ya Wanajeshi wawili wa Umoja huo kuwafyatulia Risasi waandamanaji na kuwaua watu watatu huku wengine 15 wakijeruiwa siku ya Jumapili katika Mji wa mpakani wa Kasindi.

Waandamanaji wakipinga uwepo wa majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Congo

Waliohusika katika vurugu hizo wamesimamishwa kazi  kwa muda kwani tukio hilo limewakasilisha Raia wa DRC ambao wamesema  kuwa uwepo wa Jeshi hilo nchini humo,  zaidi ya muongo mmoja haujaleta amani na wamekuwa wakiliomba Jeshi hilo kuondoka haraka iwezekanavyo.

Baada ya maandamano kwa zaidi ya wiki moja Serikali imepanga kuangazia upya hatua ya kuondoka kwa Jeshi hilo.

Leave A Reply