The House of Favourite Newspapers

Mr Eazi Aachia Ngoma Yake ya Pili Iitwayo Personal Baby Kutoka Kwenye Albamu Mpya 

0

 

STAA wa muziki kutoka nchini Nigeria, Mr Eazi ameachia ngoma yake mpya, Personal Baby ambayo ni ya pili kuachiwa kutoka katika albamu yake mpya ambayo bado hajaiachia.

 

Wimbo huo umetengenezwa na  Prodyuza Kel P ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Grammy, akiwa amewahi kufanya kazi na mastaa wakubwa nchini humo kama Burna Boy, Wizkid na Angelique Kidjo.

 

 

 

Kwa upande wa video, amesimama dairekta maarufu, Ademola Falomo ambaye amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha vionjo vya muziki wa asili wa Banku alivyoviweka Mr Eazi katika wimbo huo, vinaendana na video huzika.

 

Kwa upande wa uandishi, Mr Eazi ameshirikiana kuandika na msanii mwenzake, Teni ambapo mashairi yake yanazungumzia zaidi mapenzi, ukiwa ni wimbo wa pili baada ya Legalize, ambao unaendelea kufanya vizuri kutoka kwa msanii huyo na unaweza kuisikiliza au kuitazama kwenye majukwaa yote kwa kubofya Personal Baby

 

Leave A Reply