The House of Favourite Newspapers

DRC Yasitisha Chanjo ya Covid 19

0

SERIKALI ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeahirisha kampeni ya kutoa chanjo ya AstraZeneca.

 

Taifa hilo limepokea dozi milioni 1.7 ya chanjo hiyo dhidi ya Covid-19 na ilitarajiwa kuanza zoezi la kuchanja watu mnamo machi 15.

 

Waziri wa Afya Eteni Longondo amesema wameamua kuahirisha tarehe ya uzinduzi wa chanjo hiyo kama hatua ya tahadhari, baada ya nchi nyingine kadhaa kufanya uamuzi kama huo.

 

Waziri huyo amesema tarehe mpya ya uzinduzi wa chanjo hio itatangazwa baada ya uchunguzi wa kiserikali na wa kimataifa.

 

Denmark, Norway, Bulgaria na Iceland zimesimamisha utoaji wa chanjo hiyo juu ya hofu kuwa inasababisha kuganda kwa damu, na India imesema itafanya uchunguzi wa kina juu ya athari za baada ya chanjo.

 

Shirika la Afya Duniani WHO hata hivyo limesema chanjo hiyo ni salama, na hakuna ushahidi kuwa inasababisha madhara hayo.

 

Leave A Reply