The House of Favourite Newspapers

Dreamliner Mpya Kuanza Safari Zake ‘Soon’, Tiketi Zagombaniwa

SHIRIKA la la Tanzania (ATCL) linatarajia kuanza safari za ndege yake mpya iliyotua Jumapili iliyoipita, Dreamliner 787-8 mnamo Julai 29, mwaka huu kwenda Mwanza na Kilimanjaro kwa kishindo huku wananchi wakitiririka kukata tiketi za ndege hiyo.

Dreamliner787 ya Air Tanzania inavyoonekana kwa ndani. Hili ni daraja la Uchumi (Economy Class).

Kwa mujibu wa abiria ambao tayari wameshakata tiketi wamesema tiketi kuisha mpaka za kufikia tarehe 18 Agosti 2018 zimeshaisha tayari kutokana na wingi wa abiria wanaoendelea kumiminika kukata tiketi hizo mapema kwa ajili ya safari.

 

Kupitia akaunti yao ya Twitter, ATCL wameandika; “Wahi tiketi yako mapema kwa kutembelea ofisi zetu, tovuti (), piga 0800 110045 au wakala wa safari za anga alie karibu nawe. Kuwa wa kwanza kupanda   ya Air Tanzania kwa bei sawa na BURE. na 

Muonekano wa “Business Class”.

Wahi tiketi yako mapema kuonja asali ya anga, piga 0800 110045 au ingia kwenye tovuti yetu Ofa hii inaanza tarehe 29/07 – 25/08.

Comments are closed.