The House of Favourite Newspapers

Drogba Kuishtaki Daily Mail

0

Drogba Foundation (3)

Mwanasoka maarufu duniani, Didier Drogba pamoja na Princess Beatrice wakiwa pamoja siku ya uzinduzi wa Taasisi ya Didier Drogba mwaka 2012.

Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Daily Mail.

Hii ni baada ya gazeti hilo kuchapisha habari zinazodai kwamba kati ya pesa anazokusanya kupitia wakfu wake wa kusaidia jamii, ni chini ya asilimia moja zinazotumiwa kufaa jamii.

Drogba Foundation (5)

Taasisi ya Didier Drogba Foundation ilidhamiria kusaidia maisha ya Waafrika 10,000 kwa mwaka.

Gazeti hilo limesema ni £14,115 pekee kati ya £1.7m zinazotolewa na wachezaji nyota na wafanyabiashara ambazo husaidia watoto Afrika.

Drogba Foundation (4)Jengo la Didier Drogba Foundation.

Drogba, 38, ametoa taarifa akisema habari hizo ni za “uongo na za kumharibia sifa”.

Tume inayodhibiti mashirika ya kusaidia jamii yaliyosajiliwa Uingereza imesema inachunguza “madai ya ukiukaji wa sheria”.

Drogba Foundation (2)

Christine Bleakley na Frank Lampard wakipozi na Drogba.

Kwenye taarifa yake, Drogba amesema: “Hakuna ulaghai, hakuna ufisadi na hakuna udanganyifu.”

Drogba Foundation (1)

Drogba na mwanamuziki, Una Healy wakati wa sherehe ya uzinduzi wa taasisi hiyo.

Drogba, raia wa Ivory Coast, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Canada kwa sasa amewatuhumu wanahabari wa Daily Mail kwa kuweka hatarini maisha ya maelfu ya watoto wa Afrika.

SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply