The House of Favourite Newspapers

Droo Ndogo ya Tatu Yasubiriwa Kwa Hamu

0

 

STORI: MWANDISHI WETU, Risasi Jumamosi

WASOMAJI wa magazeti ya Global Publishers, ambao wanaendelea ku­jikusanyia kuponi kwa ajili ya Bahati Nasibu ya Shin­da Nyumba Awamu ya Pili, wanais­ubiri kwa hamu droo ndogo ya tatu inayotarajiwa kufanyika Aprili 26, mwaka huu.

Katika droo hiyo zawadi za Pikipiki, seti ya televisheni, simu za kisasa na dinner set, zitamwagwa tena kwa wasomaji watakaoibuka kidedea.

Droo hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti pendwa ya Iju­maa, Risasi, Amani, Uwazi, Ijumaa Wikienda na lile la michezo nam­bari moja Tanzania la Championi, imeshafanya droo ndogo mbili.

Akizungumza na Risasi Juma­mosi, Msomaji Hamis Juma mkazi wa Kijitonyama, Dar alisema ana­tamani Aprili 26 ifike haraka kwani ana uhakika kwamba lazima ap­ate zawadi kwani kila siku ame­kuwa akisoma magazeti ya Global Publishers na amefanikiwa kukata kuponi kibao.

“Natamani siku hiyo ifike haraka kwa sababu nimeshakata kuponi nyingi za kutosha nab ado ninaen­delea hivyo sitakosa zawadi moja­wapo kati ya pikipiki na nyinginezo maana zipo nyingi,” alisema Hamis.

Droo mbili za kwanza ambazo jumla ya wasomaji tisa wame­jishindia zawadi mbalimbali zikiwemo pikipiki mbili, televisheni flat skrini mbili, dinner set na simu za kisasa seti mbili pia, zilifanyika katika ukumbi mkubwa wa buru­dani wa Dar Live huko Mbagala Zakhem na viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Katika droo hiyo ndogo ya tatu, Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho al­isema zawadi kubwa itakuwa ni pikipiki, huku washindi wengine wakijitwalia simu za kisasa za mkononi aina ya smartphone, seti moja ya televisheni ‘flat screen’ na Dinner Set.

Leave A Reply