The House of Favourite Newspapers

DTB yamwaga manoti Ligi Kuu Bara

malinzi-mkataba-na-bank-2Malinzi (kushoto) na Mabusi wakisaini mkataba.

malinzi-mkataba-na-bank-3Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nandi Mwiyombella, Rais wa TFF, Jamal Malinzi, Ofisa Mkuu wa Mapato DTB, Joseph Mabusi, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania, Hamad Yahaya, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Tanzania, Said Mohammed, baada ya kusaini mkataba.

malinzi-mkataba-na-bank-4Malinzi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) huku Nandi (kushoto) na Mabusi wakimsikiliza kwa makini.

malinzi-mkataba-na-bank-1Mmiliki wa Klabu ya African Lyon ambaye alikuwa kama mwakilishi wa klabu zote za ligi kuu akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.

BENKI ya Diamond Trust (DTB), leo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuidhamini Ligi Kuu Bara.

Mkataba huo wenye thamani ya Sh milioni 250, unaweza kuongezwa baada ya huu wa awali kumalizika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Mapato DTB, Joseph Mabusi, alisema: “Tunayofuraha kuwa miongoni mwa wadhamini wa Ligi Kuu Bara, tutashirikiana vema na wenzetu tuliowakuta kama NHIF, Vodacom na Azam TV, lengo likiwa ni moja tu kuusogeza mbele mchezo wa soka hapa nchini.”

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi, alisema: “Tunashukuru kuona watu kama hawa wakijitokeza kuidhamini ligi yetu, tunaomba wengine kwa nafasi zao waje kwani milango ipo wazi.”

Imeandaliwa na Omary Mdose/Championi.

Comments are closed.