The House of Favourite Newspapers

Dube: Viongozi wa Azam hufurahia mafanikio ya timu zingine badala ya timu yao!

0

Sakata la mshambuliaji Prince Dube limeingia sura mpya baada ya nyota huyo raia wa Zimbabwe kudai ndani ya klabu ya Azam viongozi wa klabu hiyo hufurahia mafanikio ya timu zingine badala ya timu yao!

“Nahitaji kuchezea timu ambayo wachezaji na viongozi wana lengo moja. Viongozi wako Azam, lakini mioyo yao iko kwenye timu zingine wanazozisapoti, hizo timu zikishinda wanafurahia.

“Hili ni tatizo jingine unajua mara nyingine ni ngumu kusema vitu hivi lakini sasa tuko kwenye hali ngumu natakiwa kusema sina chaguo.

“Siwezi kuwa kwenye timu ambayo wewe unataka kushinda kitu lakini watu ambao wanawaongoza wanasapoti timu mnayoshindana nayo, ndiyo maana nataka mabadiliko niwe sehemu ambayo watu wanaowaongoza mnafikiria kitu kimoja” – Prince Dube.

Leave A Reply