The House of Favourite Newspapers

DULLAH MBABE AMTWANGA MMALAWI

Dullah Mbabe (mwenye kiduku) akimpelekesha kwa makonde Mmalawi.

Bondia Dullah Mbabe wa nchini jana alimtwanga kwa TKO raundi ya tatu, bondia  wa Malawi, Felix Mwamaso,  katika pambano lililokuwa lipiganwe kwa raundi kumi katika Uwanja wa Taifa wa Ndani jijini Dar.

 

Mmalawi (kulia) akiugulia maumivu baada ya kugongwa ngumi kali za kichwani.

Mwamaso alionekana kuzidiwa na Dullah  kuanzia raundi ya kwanza ambapo aliangushwa mara kadhaa.

 

Mwamuzi akiwaamulia baada ya kuona Dullah anataka kumdhuru  Mwamaso.

 

Mmalawi akiomba poo kwa mwamuzi.

 

Baada ya mwamuzi kumaliza pambano na kumpa ushindi wa TKO, Dullah Mbabe, Mmalawi alishindwa kutembea na kuanza kutambaa ulingoni.

 

Dullah Mbabe akivishwa mkanda baada ya kutangazwa mshindi.

 

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL   

Comments are closed.