The House of Favourite Newspapers

Duma: Mastaa Wengi Wa Filamu Ni Ombaomba

Daud Michael ‘Duma’.

MSANII wa filamu Bongo, Daud Michael ‘Duma’ ameibuka na kuwachana mastaa wenzake hasa wa filamu kuwa wengi ni ombaomba ndiyo maana sanaa hiyo imekufa.

 

Akichonga na Risasi Jumamosi, Duma alisema mastaa wa filamu wamekuwa wakipata nafasi ya kuonana na matajiri wengi lakini wamekuwa wakiishia kupiga mizinga ya fedha na kushindwa kuzungumza nao mambo muhimu ambayo yanaweza kuwasaidia katika kazi zao.

 

“Sanaa yetu imekufa kwa sababu ya wasanii wengi kuwa ombaomba kwa ajili ya matakwa binafsi, iwapo wangekuwa wanaelezea shida za filamu kwa matajiri wanaokutana nao wala sanaa yetu isingefikia hapa ilipo,” alisema Duma.

Comments are closed.